Home Uncategorized ISHU YA KUBORONGA KWA BODI YA LIGI, MASAU AIBUKA, SIMBA YATAJWA

ISHU YA KUBORONGA KWA BODI YA LIGI, MASAU AIBUKA, SIMBA YATAJWA


BAADA ya jana bodi ya Ligi kuweka usawa na kukubali kwamba wameboronga kwenye suala la kukusanya data za matokeo ya mchezo wa Stand United na Kagera Sugar kisha kuishusha Kagera Sugar kabla ya kuipanisha tena Uongozi wa Ruvu Shooting umeibukia huko.

Ofisa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire ameandika waraka huu kuhusu sakata la kuboronga kwa Bodi ya Ligi Tanzania:-

“Kumekuwepo na mjadala mzito sana kuhusu makosa yaliyofanyika, kumtangaza Kagera kuwa ndiye kashuka daraja moja kwa moja, badala ya Stand ambaye ndiye anastahili kushuka kwa mujibu wa kanuni. 

“Mjadala huu umeenda mbali kufikia kudai kwamba ni mkakati uliopangwa na TFF /TPLB ili kuihujumu Kagera Sugar,  wengine wakihoji kwamba, kwa nini kama kanuni inasema head to head, msimu wa ligi 2017, ambapo Simba na Yanga walilingana pointi mshindi alipatikana kwa tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa,  iweje msimu huu iwe tofauti, apatikane kwa matokeo yaliyowakutanisha (head to head ). 

“Head to head, inawezekana kuamua mshindi kama wakilingana pointi endapo kanuni inazungumza hivyo.

“Inawezekana msimu huu tukatumia head to head, msimu ujao tukatumia tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa, msimu mwingine tukatumia mwenye magoli mengi ya kufunga kama kanuni itazungumza hivyo.

“Kanuni zinabadilika, siyo Msaafu kwamba kilichoandikwa ni hicho hicho milele, hapana, kanuni zinabadilika kutokana na mahitaji kama itakavyoamriwa.

“Kwa hiyo, kanuni za 2017 kama kanuni ilisema tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa, msimu huu ikasema head to head, ni sawa, haihitaji kulinganisha kanuni ya mwaka mwingine na mwingine kwani zinabadilika hizi kanuni.

“Ukweli ni kwamba, kanuni zilizotumika mwaka huu, kanuni ya 7 (Mshindi), baada ya timu kulingana pointi, mshindi atapatikana kwa tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa  ,kanuni ya 7(3).

“Kipengele cha kuamua mshindi head to head kwenye kanuni kipo, ni cha 5, kingetumika kama manne ya mwanzo yangezipa sifa sawa timu hizo.

“Kipengele hicho cha tano katika kanuni hiyo ya 7, hakiwezi kutumika kwa kuwa, kipengele cha tatu kilikuwa kinampata mshindi.

“Kilichotokea kwa Kagera na Stand, nadhani ni mapungufu ya kawaida, ya Kibinadamu, yaliyofanywa na mtu mmoja, siyo ya makusudi, siyo ya kupangwa kama inavyotafsiriwa.

“Nashukuru kwamba, baada ya uongozi wa juu wa TFF na TPLB kujiridhisha kwamba, Stand ndiye mwenye sifa ya kushuka, haraka walirekebisha na kutangaza mabadiliko hayo.

“Hata huyo mmoja aliyefanya hayo makosa, naamini haikuwa dhamira yake kufanya hivyo, ni makosa ya Kibinadamu, nina hakika baada ya kugundulika hivyo, hata yeye ameumia, kusononeka na kutaabika sana!

“Tusihukumu, kabla ya hukumu, tutahukumiwa.

“Tusamehe, tuachane na hili, tujadili mengine ya kuifanya ligi yetu msimu ujao, iwe bora zaidi.

“Ambaye hajawahi kufanya kosa lolote, awe wa kwanza kumpiga MAWE.Ahsante, Masau Kuliga Bwire – Mzalendo amemaliza.

SOMA NA HII  NYOTA WAPYA WA YANGA WAWEKA REKODI YAO