Home Uncategorized YANGA WAIPANGIA KIKOSI CHA MAUAJI AZAM FC

YANGA WAIPANGIA KIKOSI CHA MAUAJI AZAM FC

UONGOZI wa Azam FC, umesema kuwa wametumia mbinu moja kubwa ikiwa ni pamoja na mchezo wao dhidi ya Yanga kuandaa kikosi cha mauaji dhidi ya Lipuli.

Mchezo wa mwisho wa Azam kwenye ligi walicheza na Yanga na kuibuka na ushindi wa mabao 2-0, hali iliyowapa kujiamini wachezaji kuelekea fainali ya FA.

Azam itamenyana na Lipuli kwenye fainali ya kombe la FA utakaochezwa uwanja wa Ilulu, mkoani Lindi na bingwa atawakilisha nchi kwenye michuano ya kimataifa.

Akizungumza na Saleh Jembe, Idd Cheche, kocha wa Azam FC amesema kuwa maandalizi yalianza mapema na mechi zake za mwisho wa ligi amezitumia kutengeneza kikosi cha mauaji dhid ya Lipuli hivyo hana mashaka katika hilo.

“Tulipoteza uwezo wa kutwaa ubingwa wa ligi, nguvu zetu tukazipeleka kwenye maandalizi ya kutwaa kombe la FA, hivyo michezo yetu yote ya mwisho kwenye ligi tulikuwa tunafanya maandalizi ya fainali.

“Tunajua mchezo utakuwa mgumu, ila tupo tayari kufanya vizuri na kutwaa ubingwa kwa kuwa tumejipanga na tuna imani ya kushinda, mashabiki watupe sapoti katika mchezo wetu,” amesema Cheche.

SOMA NA HII  SIMBA; KUTOLEWA MAPEMA LIGI YA MABINGWA NI SOMO KWETU