Home Uncategorized AZAM YALETA CHANGAMOTO KWA SIMBA

AZAM YALETA CHANGAMOTO KWA SIMBA


Kocha Mkuu wa timu ya Azam, Ettiene Ndayiragije raia wa Burundi amepanga kukiboresha kikosi chake kuelekea msimu ujao wa Ligi Kuu Bara kwa kuwasajili wachezaji wapya wanne ambao wataenda kusaidiana na Obrey Chirwa.

Chirwa ambaye hivi karibuni alisaini mkataba mpya wa mwaka mmoja wa kuendelea kusalia kutumikia Azam ambayo msimu ujao itashiriki Kombe la Shirikisho Afrika anatarajiwa kuonyesha uwezo wa juu sana msimu ujao.

Ofisa Habari wa Azam, Jaffar Idd alisema kuwa kocha amepanga kuongeza wachezaji wanne ambao anaamini wakisaidiana na Chirwa watapata matokeo mazuri.

“Mwalimu alisema anataka wachezaji wanne ambapo mmoja tushampatia lakini wengine tunaendelea kushughulika nao kusajiliwa, kwa sasa hatuwezi kutaja ni nchi gani wanatoka mpaka tukamilishe kazi hiyo, kambi rasmi tumepanga kuweka tukishatoka katika michuano ya Kagame,” alisema Idd.

SOMA NA HII  MTUPIA MABAO NAMBA MOJA NDANI YA YANGA KUSEPA MAZIMA