Home Uncategorized BARCELONA KUIPASUA MANCHESTER UNITED WAKIIKOSA SAINI YA GRIEZMANN

BARCELONA KUIPASUA MANCHESTER UNITED WAKIIKOSA SAINI YA GRIEZMANN


IMEELEZWA kuwa, Marcus Rashford atakuwa mbadala ndani ya kikosi cha Barcelona iwapo watafeli kuipata saini ya Antoine Griezmann ama Neymar Jr.
Barcelona kwa sasa wanaangalia namna ya kumpata mchezaji atakayekuwa mbadala wa mshambuliaji wa kimataifa wa timu ya Taifa ya Uruguay, Luis Suarez msimu huu.
Rashford kwa sasa imeelezwa kuwa hana furaha ndani ya kikosi cha Manchester United hivyo Barcelona watatumia njia hiyo kama kigezo cha kumpata haraka kama dili la kuipata saini ya Griezmann ambaye amesema kuwa anaondoka Atletico Madrid msimu huu ama Neymar anayekipiga PSG. 


SOMA NA HII  YANGA YAPIGA HESABU ZA KIMATAIFA KUBORESHA KIKOSI CHAO