Home Uncategorized CAF YAITISHA KIKAO CHA DHARULA

CAF YAITISHA KIKAO CHA DHARULA

Rais wa Shirikisho la Soka barani Afrika CAF, Ahmad Ahmad ameitisha kikao cha dharura cha Kamati ya Utendaji ya shirikisho hilo kufuatia sintofahamu katika mchezo wa pili wa fainali ya Klabu Bingwa Afrika.
 Mei 31 nchini Tunisia kati ya wenyeji Esperance de Tunis na Wydad Casablanca ya Morocco mchezo uliisha kwa sintofahamu kufuatia klabu ya Wydad kugomea kuendelea na mchezo baada ya bao lao la kusawazisha kukataliwa katika dakika ya 62 ya mchezo.
Taarifa ya CAF imesema kuwa kikao hicho kitafanyika Juni 4, ambapo ajenda kuu itakuwa ni juu ya sheria zanazopaswa katika kutatua sintofahamu ya mchezo huo.

Kwenye mchezo huo, Wydad walisawazisha bao, ambalo lingeufanya mchezo kuwa sare ya 1-1 lakini mwamuzi alikataa bao hilo na halikurudiwa katika teknolojia ya usaidizi wa video VAR kwa kile mwamuzi alichokidai kuwa mashine kuharibika.
Baada ya Wydad kugoma kuendelea na mchezo, mwamuzi alimaliza mchezo na kuipa ushindi wa bao 1-0 klabu ya Esperance pamoja na ubingwa wa michuano hiyo.
SOMA NA HII  JOB AMTULIZA MAZIMA CHE MALONE