Home Uncategorized CRISTIANO RONALDO HANA MPANGO WA KUSTAAFU TIMU YA TAIFA

CRISTIANO RONALDO HANA MPANGO WA KUSTAAFU TIMU YA TAIFA


CRISTIANO Ronaldo mchezaji wa timu ya Taifa ya Ureno amesema kuwa bado ana imani ya kuitumikai timu yake ya Taifa kwa kubwa bado ana nguvu.
Licha ya kuwa na umri wa miaka 34 bado amekuwa ni msaada ndani ya kikosi cha Ureno licha ya kushindwa kufanikiwa kutwaa kombe la Dunia mwaka jana.
Ronaldo ambaye mwaka 2018 alishinda taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa na Real Madrid kwenye hotuba yake aliyoitoa wengi walitambua kwamba hana hesabu za kubaki ndani ya kikosi hcho na kweli imetokea kwa kuhamia kikosi cha Juventus kwa sasa.
Kwa sasa mipango yake ni kuona anapata nafasi ya kushirki kwenye michuano ya kombe la Dunia mwaka 2022 ambapo atakuwa na umri wa miaka 37 nchini Qatar.
Malengo yake ni kuona anacheza mpaka akiwa na umri wa miaka 40 na anaimani ataifikisha timu hatua ya fainali licha ya mwaka jana kushindwa kufanya hivyo.
SOMA NA HII  NAMUNGO KUSAJILI WACHEZAJI 20