Home Uncategorized ETO’O: STARS ITAFANYA MAAJABU AFCON

ETO’O: STARS ITAFANYA MAAJABU AFCON


NGULI wa soka wa Cameroon, Samuel Eto’o ameweka wazi kuwa anaamini timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars itafanya kweli katika mashindano ya Kombe la Afrika ‘Afcon’ mwaka huu.

Stars inatarajiwa kushiriki Afcon ambayo imepangwa kuanza kutimua vumbi Juni 21 hadi Julai 19, mwaka huu nchini Misri.

Eto’o ni mshindi mara mbili wa Afcon mwaka 2000 na 2002 akiwa na kikosi cha Cameroon, pia amewahi kuwa mchezaji bora wa Afrika mara nne, mshindi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya ‘Uefa’ mara tatu aliyotwaa akiwa na Barcelona na Serie A pia ana mataji mengine mbalimbali.

Mshambuliaji huyo ambaye pia amewahi kuichezea Chelsea, alizungumza na Championi Jumamosi na kushangaa kwa Stars kukaa miaka 39 bila kufuzu Afcon wakati kuna wachezaji wenye viwango vya juu.

Eto’o ambaye kwa sasa yupo nchini katika mashindano ya Castle Lager 5 Aside akiwa ni balozi wa ukanda wa Afrika alisema anafurahi kuona Tanzania imefuzu kucheza Afcon huku akiipa nafasi Stars kufanya vizuri katika mashindano hayo.

“Nashangaa kwa nini Tanzania imekaa muda mrefu bila kushiriki Afcon, nafikiri sasa huu ni wakati wao na nina imani watafanya vizuri, “ alisema Eto’o.

SOMA NA HII  HESABU ZA SIMBA KWA YANGA ZIPO NAMNA HII KESHO