Home Uncategorized Hakuna uhakika wa Zana

Hakuna uhakika wa Zana

Kandanda inatambua kuwa kuna uwezekano mkubwa sana beki wa kulia wa Simba Sc aliyekuja kuziba nafasi ya Shomari Kapombe, hatarudi tena.

Zana Coulibaly aliaminika kuwa ni mbadala wa Shomari Kapombe ambaye aliumia akiwa na kikosi cha Taifa Stars, ameshindwa kuwashawishi Simba ili aongezewe mkataba. Tetesi hizi zimetua katika Meza ya Uhamisho ya Kandanda baada ya Simba kuanza kutoa taarifa za usajili wao.

Beki huyu mwenye mbwembwe nyingi nje na ndani ya uwanja lakini pia msaurifu wa majukumu yake awepo uwanjani, kwa kiwango fulani ameisaidia sana Simba katika kutengeneza/kutoa pasi za mwisho za goli.

Ingawa uongozi wa Simba umekataa kuhusu tetesi za Zana kuachwa ni za uzushi, lakini ni wazi Zana kubaki Simba ananafasi ndogo sana.

Kandanda inaendelea kufuatilia kujua pia wachezaji gani wanaondoka, na nani pia atachukua nafasi ya Zana kwakuwa hata Kapombe pia bado hajapona.

The post Hakuna uhakika wa Zana appeared first on Kandanda.

SOMA NA HII  KIKOSI CHA YANGA KITAKACHOANZA LEO DHIDI YA NAMUNGO FC UWANJA WA TAIFA