Home Uncategorized HATMA YA AJIBU KUJIUNGA NA SIMBA HII HAPA

HATMA YA AJIBU KUJIUNGA NA SIMBA HII HAPA

MENEJA wa nyota wa Yanga, Ibrahim Ajibu, Athuman Ajibu amesema kuwa kwa sasa suala la timu atakayojiunga mteja wake Ajibu bado ni pasua kichwa hivyo kesho anaamini mipango itakuwa imekamilika.

Ajibu alikuwa anahitajika kujiunga na TP Mazembe aliamua kuzingua kwa kile kilichoelezwa kwamba ni dau dogo na sasa imeelezwa kuwa hana nafasi ndani ya Yanga.

Akizungumza na Salehe Jembe, Ajibu amesema kuwa kwa sasa mambo bado hayajakaa sawa mpaka kesho itafahamika.

“Mimi ninachoamini ni kwamba kambi popote anaweza kutua Simba ama akabaki Yanga. ila ishu ya TP Mazembe hiyo imeshabuma hatakwenda huko, mpaka Juni 30 nitakuwa nimekamilisha utaratibu wa timu yake,” amesema

Imeelezwa kuwa tayari Ajibu amemalizana na Simba na anachosubiri kwa sasa ni kutambulishwa rasmi a
ndani ya kikosi hicho.

SOMA NA HII  MAYANGA YUPOYUPO SANA KWENYE UBORA WAKE