Home Uncategorized HOTEL YA KITALII YA SNOWCREST ARUSHA YADAIWA KUFILISIWA

HOTEL YA KITALII YA SNOWCREST ARUSHA YADAIWA KUFILISIWA


HATIMAYE  hoteli ya kitalii ya Snowcrest,iliyopo eneo la Ngulelo jijini Arusha, imefilisiwa rasmi  baada ya kushindwa kujiendesha kutokana na madeni mbalimbali makubwa inayodaiwa na taasisi za kifedha na watu binafsi yanayofikia kiasi cha sh. bilioni 14.

Hotel hiyo ambayo iliwahi kuzinduliwa kwa mbwembwe na rais wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete, inamilikiwa na mfanyabiashara William Mollel ambaye aliinunua kutoka kwa mfanyabiashara aliyetambulika kwa jina la Tarimo.

Majira ya alfajiri kampuni ya udalali iliyopewa mamlaka na mahakama chini ya usimamizi wa askari polisi wenye silaha, imekomba kila kitu katika hoteli hiyo yakiwemo magodoro, mapazia, samani mbalimbali, viti, TV, vyombo, vitanda, kompyuta, mashuka, taulo na kadhalika,  na kuviacha vyumba zaidi ya 100 vikiwa havina kitu.


Kwa mujibu wa kampuni hiyo ya udalali, hata kama vitu vyote vilivyotolewa vikiuzwa, uwezekano wa kufidia madeni hayo bado ni mdogo na hivyo hatua ya kuiomba mahakama kuuza jengo zima inaweza kufikiwa muda wowote.

CHANZO: JAMII FORUM

SOMA NA HII  HALI MBAYA YA MAHUJAA FC YAMBAGIHA MANYANGA BARESI