Home Uncategorized HUU SASA NI MSALA ZAIDI, NYOTA WAWILI TEGEMEO KUIKOSA ALGERIA JUMATATU –...

HUU SASA NI MSALA ZAIDI, NYOTA WAWILI TEGEMEO KUIKOSA ALGERIA JUMATATU – VIDEO


Viungo nyota wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Mudathir Yahya na Erasto Nyoni hawatakuwa sehemu ya kikosi cha timu hiyo kwenye mechi ya Kombe la Mataifa Afrika (Afcon) mbele ya Algeria itakayopigwa julai Mosi majira ya saa 4 usiku.

Nyota hao watakosa mechi hiyo ya Stars ya mwisho katika Afcon mbele ya Algeria inayoongozwa na kiungo wa Manchester City, Riyad Mahrez kutokana na sababu mbalimbali.

Mudathir yeye atalikosa pambano hilo la Algeria kutokana na kuwa na kadi tatu za njano wakati kiraka Nyoni kwa upande wake atakosekana kutokana na kuumia kwenye mechi na Kenya ambayo Stars ilipoteza kwa mabao 3-2.

Mwandishi wetu alikuwepo nchini Misri Saleh Ally kutoka ndani ya kambi ya timu hiyo ni kuwa wachezaji hao watakosa pambano hilo huku wachezaji ambao hawakucheza mechi za awali dhidi ya Senegal na Kenya ndiyo watapewa nafasi kwenye mechi hiyo.

Kikosi hicho cha Stars kinachonolewa na Mnigeria Emmanuel Amunike kwenye mechi hiyo kitaingia kikiwa cha kupoteza kutokana na matokeo mabaya ambayo walikuwa nayo katika mechi zake mbili za awali.

Stars hadi sasa hawana pointi yoyote baada ya kufungwa mechi na Senegal mabao 2-0 na Kenya 3-2.

SOMA NA HII  KICHUYA AWEKWA MTEGONI SIMBA - VIDEO