Home Uncategorized KAZI IPO LEO FAINALI FA ILULU, LIPULI VS AZAM FC

KAZI IPO LEO FAINALI FA ILULU, LIPULI VS AZAM FC

LEO Azam FC itamenyana na Lipuli fainali ya kombe la Shirikisho mchezo utakaochezwa uwanja wa Ilulu, Lindi ikiwa ni mara ya kwanza kwa timu hizi kukutana fainali.

Azam FC ilitinga hatua ya fainali baada ya kushinda bao 1-0 dhidi ya KMC mchezo wa nusu fainali uliochezwa uwanja wa Chamanzi.

Lipuli ilitinga hatua hii baada ya kushinda kwa mabao 2-0 dhidi ya Yanga mchezo wa nusu fainali uliochezwa uwanja wa Samora, Iringa.

Hii ni mara ya kwanza kwa Lipuli kutinga fainali huku Azam FC ikiwa ni mara ya pili mara ya kwanza ilikuwa msimu wa mwaka 2015/16 ilifungwa mabao 3-1 na Yanga uwanja wa Taifa.

SOMA NA HII  JINSI PACOME ALIVYOINUSURU YANGA KWENYE HATARI YA WARABU