Home Uncategorized KUMBE HATA HUYU HAJASAINI BHANA…

KUMBE HATA HUYU HAJASAINI BHANA…


Taarifa za uhakika zinasema kuwa kwamba mchezaji Ibrahim Ajibu hajasaini YANGA, na kwa siku tatu sasa hapokei simu za viongozi wa timu hiyo. 

Kwa mujibu wa chanzo chetu cha kujiridhisha kimesema mpaka sasa Yanga wameshindwa kufikiana mwafaka na Ajibu ambaye imeonekana dau walilompatia ameshindwa kukubaliana nalo.

Chanzo hicho kimesema Yanga na Ajibu wamekuwa hawana maelewano hivi sasa kufutia mchezaji mwenyewe kukataa ofa waliyompa na badala yake amekuwa akihitaji cha juu zaidi.

Ikumbwe Ajibu aliyetoka Simba misimu miwili nyuma ameanza kuhusishwa kujiunga na Simba kwa ajili ya kutoa huduma kwa msimu ujao.

Taarifa zilizopo ni kwamba Ajibu amekuwa hapatikani katika simu yake mkononi ikiwa ni moja ya ishara ya kutoelewana na mabosi wake juu ya kiasi cha fedha wanachotaka kumpatia ili asaini mkataba mpya.

Awali kulitolewa taarifa za kuwa ameongeza mkataba wa miaka miwili lakini uhakika uliopo ni bado.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURAAA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMATANO