Home Uncategorized MANCHESTER UNITED KUMLIPA MKWANJA MREFU DAVID de GEA

MANCHESTER UNITED KUMLIPA MKWANJA MREFU DAVID de GEA

Kwa mujibu wa The Sun, Manchester United wapo tayari kumpa David de Gea pauni 20m kama mlinda mlango huyo atahamia Paris Saint-Germain katika usajili wa majira ya joto.
Fedha hizo ni sehemu ya mauzo ya kipa huyo ambapo mmoja wa mabosi wa mashetani hao wekundu amesema wapo tayari kupokea ofa kuanzia paundi 60m kutoka kwa mabingwa hao wa Ligue 1
Mlinda mlango huyo mwenye umri wa miaka 28 anahitaji kuondoka ndani ya klabu hiyo msimu ujao licha ya mabosi kuhitaji kupata huduma yake na hawapendi kuona anaondoka bure.
United wapo tayari kumpa kiasi cha Euro milioni 20 De Gea ambaye wengi wanapenda kumuita mikono ya dhahabu kabla mkataba wake haujameguka.
De Gea anajua kwamba yupo kwenye hesabu za wachezaji ambao wanahitajika kupewa mkataba mpya licha ya nia yake ya kutaka kuondoka ila lengo la mabosi wa United ni kuona kwamba haondoki bure.
Imeelezwa kuwa De Gea anawindwa na PSG ili akawe mlinda mlango namba moja akachukua gloves za Gianluigi Buffon ambaye amemaliza mkataba.
SOMA NA HII  KESHO NDANI YA SPOTI XTRA JUMAPILI USIPANGE KUKOSA NAKALA YAKO