Home Uncategorized MIDO WA SINGIDA KUBEBA MIL 20 YANGA

MIDO WA SINGIDA KUBEBA MIL 20 YANGA


IMEFAHAMIKA kwamba mido mpya wa Yanga, Kenny Ally ambaye anaichezea Singida United atalamba milioni 20 ikiwa ni sehemu yake ya usajili.

Yanga watampata mido huyo wa Singida kilaini kabisa kutokana na usajili wake kukamilishwa kila kitu na Mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba.

Taarifa kutoka ndani ya Yanga ambazo Championi Jumatatu, limezipata ni kuwa kiungo huyo atasaini kwa kiasi hicho ambacho chote atakitoa Mwigulu.

“Kiasi hicho cha fedha ni kweli kabisa ambacho ndiyo atachukua Kenny baada ya kutua Yanga ikiwa sehemu ya dau lake kumhamisha kutoka Singida United.

“Kila kitu kuhusiana na yeye kusaini Yanga kinaenda sawa ambapo muda wowote atatambulishwa kama mchezaji mpya akiungana na hawa ambao wamesajiliwa hadi sasa,” kilisema chanzo hicho.

Championi Jumatatu lilimtafuta Mwigulu ambapo alisema: “Mimi nitamsajili mchezaji mmoja kama sehemu yangu ya mchango kwa Yanga. Dau ambalo mchezaji huyo nitamsajili hapa Yanga ni kama lile ambalo alichukua Feisal Salum ‘Fei Toto’ wakati akitua hapa, lakini siwezi kusema ni kiasi gani.”

SOMA NA HII  BAADA YA KUBEBA KOMBE..DILUNGA AMEFUNGUKA HAYA SIMBA..!!