Home Uncategorized Mimi ni shabiki wa Mtibwa na siyo Simba-Juma Kaseja

Mimi ni shabiki wa Mtibwa na siyo Simba-Juma Kaseja

Wakati watu wengi wakiamini Juma Kaseja ni shabiki wa Simba Sc kutokana na yeye kucheza kwa muda mrefu katika klabu hiyo ya Kariakoo, leo amedhibitisha rasmi kuwa yeye siyo shabiki wa Simba.

“Mimi siyo shabiki wa Simba SC, wakati mimi naanza kudaka timu ambayo ilikuwa juu ni Mtibwa Sugar. Ndiyo timu ambayo nilianza kuipenda”.

“Kuna watu hawajui , mimi nimeshawahi kudaka Mtibwa Sugar kwenye mechi moja dhidi ya Yanga. Miaka ya 2000 ndiyo miaka ambayo Mtibwa Sugar ikibeba ubingwa mara mbili mfululizo”. Alidai golikipa huyo wakati anazungumza na kituo cha radio cha East Afrika Radio.

“Mtibwa ndiyo sehemu ambayo nilitamani kucheza kwenye maisha yangu ya soka yote. Natamani kwenda kumalizia maisha yangu ya mpira kwenye klabu hiyo ya Mtibwa Sugar “- alimalizia golikipa huyo wa zamani wa Yanga na Simba.

The post Mimi ni shabiki wa Mtibwa na siyo Simba-Juma Kaseja appeared first on Kandanda.

SOMA NA HII  WAPINZANI WA YANGA KIMATAIFA WANYAKA MAFAILI YANGA WANA KAZI YA ZIADA KESHO