Home Uncategorized NDEMLA: NITASAINI YANGA

NDEMLA: NITASAINI YANGA

KIUNGO mshambuliaji wa timu ya Simba, Said Ndemla amesema kuwa anahitaji kupata changamoto mpya msimu ujao hivyo kwa sasa anafikiria kwenda kucheza nje ya nchi msimu ujao ikishindikana atasaini hata Yanga.

Ndemla msimu uliopita amekuwa na changamoto ya kupata namba ndani ya kikosi kilichotwaa ubingwa kwa mwaka 2018/19 hali iliyofanya asionyeshe yale makeke waliyozoea mashabiki.

“Nina mpango wa kwenda kucheza nje ya nchi hivyo nasubiri kuona namna gani mipango itajipa, ila kama huko itashindikana nitazungumza na viongozi wangu wa Simba kama watahitaji kuongeza mkataba nami nitasaini hata Yanga pia endapo watakidhi masharti na vigezo,” amesema.

Ndemla amekuwa akihusishwa kujiunga na Yanga na uongozi wa Yanga umesema kuwa suala la usajili lipo mikononi mwa kocha Mwinyi Zahera.

SOMA NA HII  KOCHA SIMBA AWAOMBA WATANZANIA KUENDELEA KUCHUKUA TAHADHARI DHIDI YA CORONA