Home Uncategorized NIYONZIMA AVUNJA UKIMYA SIMBA

NIYONZIMA AVUNJA UKIMYA SIMBA


Kiungo machachari wa Simba, Mnyarwanda Haruna Niyonzima, amevunja ukimya kuwa mpaka sasa uongozi wa timu hiyo haujazungumza naye ishu yoyote ya kuongeza mkataba na kwamba hilo halimtishi kwani ana ofa kibao.

Niyonzima alijiunga na Simba misimu miwili iliyopita akitokea Yanga, alianza kazi Msimbazi kwa kusuasua kutokana na majeraha kabla ya kuibuka hivi karibuni na kuonyesha kiwango kizuri.

Kwa sasa mkataba wake Msimbazi umemalizika. Akizungumza na Championi Jumamosi, Niyonzima alisema, anapenda kuendelea kucheza Simba licha ya kuwa mkataba wake umekwisha na hajaambiwa lolote na viongozi wa timu hiyo.

Alisema hata kama Simba hawatampa mkataba mwingine haina shida kwani ana ofa nyingi ambazo amezipata. “Mimi ningependa sana kuwepo Simba lakini kwa sasa napata kigugumizi kusema lolote kwa kuwa mkataba umeisha na sijaambiwa lolote na uongozi.

“Watu wajue kuwa hapa (Tanzania) pameshakuwa kama nyumbani na nisingependa kuondoka, lakini itategemea uongozi unasemaje maana mwisho wa siku namaliza mkataba kwa hiyo siwezi kung’ang’ania kama wao hawanihitaji,” alisema Niyonzima.

SOMA NA HII  KIUNGO WA SIMBA ATIBUA DILI LA NYOTA WA RWANDA KUTUA YANGA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here