Home Uncategorized NYOTA WA MWADUI AIYEE AWAAMBIA YANGA WAPELEKE MKWANJA MREFU

NYOTA WA MWADUI AIYEE AWAAMBIA YANGA WAPELEKE MKWANJA MREFU

NYOTA wa Mwadui FC, Salum Aiyee amesema kuwa anatazama timu yenye mkwanja mrefu ili asaini kwani ofa alizonazo mkononi kwa sasa ni nyingi.

Akizungumza na Salehe Jembe, Aiyee amesema kuwa amekuwa akizungumza na viongozi wengi wa timu mbalimbali ambao wanahitaji saini yake hivyo kikubwa kwake ni maslahi kwanza.

“Mimi najua kwamba timu yangu iliyonitambulisha kwa mashabiki ni Mwadui ila kama ofa zilizopo mkononi zikiwa na maslahi zaidi ya hapa ni lazima niondoke tu hamna namna.

“Mchezaji ni kama mfanyabiashara, yeye anaangalia faida hivyo kwa timu yenye maslahi mazuri ninakwenda na miongoni mwa timu ambazo ofa zao zipo mkononi ni Yanga, sio hao pekee wapo wengi wamekuja,” amesema Aiyee.

Aiyee ni mzawa mwenye mabao 18 akiwa ni kinara kwa wazawa, wikiendi iliyopita alitimiza majukumu yake kwa kuiokoa timu yake kushindwa kushuka daraja baada ya kufunga mabao 2 kwenye ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Geita.

SOMA NA HII  GUARDIOLA:TULISTAHILI KUSHINDA ILA NDO HIVYO TENA