Home Uncategorized RASMI HARUNA NIYONZIMA AACHANA NA SIMBA

RASMI HARUNA NIYONZIMA AACHANA NA SIMBA

KIUNGO mshambuliaji wa Simba, Mnyarwanda, Haruna Niyonzima, amewaaga mashabiki wa timu hiyo na kuwashukuru kwa yote waliyoshirikiana kwa kipindi cha misimu miwili ndani ya klabu hiyo.

Mkataba wa Niyonzima wa miaka miwili na Simba umemalizika hivi karibuni huku kukiwa hakuna dalili zozote za kuongezewa mkataba mpya na uongozi wa timu hiyo.

Ikumbukwe kuwa, kiungo huyo alijiunga na Simba msimu wa 2017/18 akitokea Yanga ambayo aliitumikia tangu msimu wa mwaka 2011 akitokea APR ya Rwanda.

Kupitia akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa Instagram, Niyonzima aliandika ujumbe mfupi wenye maneno ya kuwaaga mashabiki wa Simba.

Kiungo huyo mwenye udambwidambwi uwanjani, ujumbe wake ulisomeka hivi: “Nawashukuru kwa kumbukumbu tulizoweka pamoja, kadiri muda unavyokwenda ndiyo nitaweka wazi sehemu nitakayokwenda.”

Ikumbukwe Championi iliweka wazi mapema hatima ya mchezaji huyo ndani ya kikosi hicho kufuatia viongozi wa juu kunishikiza kutoongezewa mkataba mpya kutokana na madai ya kuwa msumbufu.

SOMA NA HII  SERIKALI YAIPA BARAKA STARS, WAZIRI AIKABIDHI BENDERA