Home Uncategorized RASMI WACHEZAJI WATATU WAPIGWA PINI SIMBA

RASMI WACHEZAJI WATATU WAPIGWA PINI SIMBA


ERASTO Nyoni, beki kiraka wa Simba rasmi ameongeza mkataba wa miaka miwili kuendelea kuitumikia klabu hiyo.

Nyoni anakuwa ni mchezaji wa tatu kwa Simba kutangazwa kwamba ameongeza mkataba wa kuitumikia klabu hiyo ambayo maskani yake yapo mitaa ya Msimbazi, Dar.

Wachezaji wengine ni pamoja na John Bocco ambaye ameongeza mkataba wa miaka miwili pamoja na mlinda mlango Aishi Manula ambaye ameongeza mkataba wa miaka mitatu na wote walisaini kabla ya kwenda Misri kushiriki michuano ya Afcon.

SOMA NA HII  AZAM FC YAMALIZANA NA MAJEMBE MAWILI FASTA, MMOJA NI MFUMANIA NYAVU KIMATAIFA