Mtandao maarufu wa The Sun wa nchini Uingereza umeripoti kuwa klabu nne zinahitaji huduma ya Mtanzania Mbwana Samatta (26) anayeichezea klabu ya KRC Genk ya Ubeligiji.
Aston Villa(Timu iliopanda ligi kuu msimu huu), Leicester, Watford na Burnley ni miongoni mwa klabu ambazo zimetenga kitita cha fedha kupata saini ya Samatta.
Samatta amekuwa na msimu wenye mafanikio baada ya kuifungia mabao 23 klabu hiyo ambayo ilitwaa kombe la ligi yao. Pia aliibuka mfungaji bora wa kutoka Afrika katika ligi hiyo.
Mwenyewe amesema mara nyingi anatamani sana kucheza Uingereza, na huenda hii ikawa nafasi yake muhimu kucheza EPL. Lakini swali kubwa jee yupo tayari kuacha kucheza Ligi ya Mabingwa ya ulaya kwaajili ya EPL?
The post Samatta anatafutwa EPL appeared first on Kandanda.