Home Uncategorized SERIKALI YAONGEZA MAKALI USIMAMIAJI WA TPL KWA WACHEZAJI WA KIGENI

SERIKALI YAONGEZA MAKALI USIMAMIAJI WA TPL KWA WACHEZAJI WA KIGENI


KUELEKEA kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2019/20 Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa, na Michezo, Dr.Harrison Mwakyembe amesema kuwa wachezaji wa kigeni watakaopata nafasi ya kucheza hawatazidi watano.

Sheria hii haitaangalia ukubwa wa timu iwe Yanga ama Simba, Lipuli, Azam FC na nyingine zote lazima zifuate.

Mwakyembe ameyasema hayo leo kwenye hotuba ya
ke ukumbi wa Diamond Jubilee ambapo kulikuwa na Tamasha la Kubwa Kuliko maalumu kwa ajili ya kuichangia timu ya Yanga kupata fedha za kujiendesha.

“Msimu ujao nataka kuona sheria zinabadilika hasa kwa wachezaji wa kigeni ambao watacheza ligi, ukisajili wachezaji 100 wa kigeni hatuna tatizo ila watakaocheza uwanjani hawatazidi watano ama wanne, na hili ninalisimamia kwa ukaribu.

“Sheria zipo na hazifuatwi hivyo hakutakuwa na ruhusa kwa timu ambayo haina timu ya vijana kushiriki Ligi Kuu Bara, tunataka tujenge timu bora ya Taifa hivyo lazima uwekezaji uwe mkubwa,” amesema Mwakyembe.

SOMA NA HII  UCHAWI WENU ULIWAKIMBIZA VODACOM, MKAWALILIA, WAMERUDI SASA TAFUTENI TIBA