Home Uncategorized SHAHIDI AOMBA MAJI MAHAKAMANI KESI YA AVEVA

SHAHIDI AOMBA MAJI MAHAKAMANI KESI YA AVEVA


SHAHIDI namba tano, Jovin Kalinga ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar kuwa, alikuwa anafahamiana na kiongozi wa zamani wa Simba, Zacharia Hans Pope na ndiye aliyemueleza kuwa Simba kuna kazi.

Wakati shahidi huyo akiendelea kutoa ushahidi mbele ya mahakama jana, katikati aliomba apewe maji ambapo Hakimu Mkazi Mkuu wa mahakama hiyo, Thomas Simba, alimpa nafasi ya dakika moja kunywa maji kisha kuendelea kutoa ushahidi wake.

Shahidi huyo alikuwa akitoa ushahidi wa kesi inayowakabili waliokuwa viongozi wa Simba Evans Aveva, Godfrey Nyange Kaburu na Hans Pope.

Kalinga aliiambia mahakama hiyo kuwa: “Kabla sijafanya kazi na Simba, nilikuwa nafahamiana na Hans Pope kwa sababu niliwahi kufanya naye kazi hapo awali.

“Hans Pope alinieleza Simba kuna kazi, hivyo niwasiliane na viongozi. Baada ya kuwasiliana, bosi alikuja na nyaraka za Simba na kunikabidhi kuwa mimi nitashughulikia kila kitu kuhusu mzigo wa Simba tena kwa maandishi.

“Nikaanza kushughulikia zile nyaraka kwa kupitia mfumo ambao unaunganishwa na TRA na katika zile nyaraka kulikuwa na invoice (Ankara) ambayo ilikuwa ya dola 40,577, zilipofanyiwa assessment (tathmini) Simba ikatakiwa kulipa Sh milioni 82 na kila kitu kikawa kimekamilika.

“Tulipoenda kutoa mzigo bandarini, incharge (msimamizi) alituambia mzigo umezuiliwa ambapo tukiwa hapo, ikapigwa simu na Salim (Try Again ambaye ni kiongozi wa Simba) kuwa mzigo uachwe kwanza, wanaenda kufuatilia Takukuru.

“Mimi na Mkurugenzi wa WAFEM Limited, Levinson Kasulwa, tulienda kuhojiwa Takukuru na nyaraka zote za faili la Simba, tukakuta zimefanana isipokuwa kiasi cha fedha kwenye zile ankara zilikuwa tofauti, ya kwetu ilikuwa dola 40,577, ile ya pili ni dola laki moja naa.

“Baadaye kiongozi wa Simba, Salim alipiga simu twende TRA sababu wamemalizana na Takukuru na mwanasheria wa TRA alisema invoice ya pili ambayo ilikuwa na dola laki moja naa (zaidi kidogo ya hizo), ndiyo ilifanyiwa kazi na ambao waliipeleka hiyo invoice TRA walikuwa ni Simba.”

Shahidi huyo aliiambia mahakama kuwa mzigo wa Simba ulitoka bandarini Machi 22, 2019. Malipo ya awali ya invoice ya kwanza ambayo ilizuiliwa ililipwa Aprili 5, 2017.

SOMA NA HII  SIMBA YAWAITA MASHABIKI,KICHAPO MBELE YA PRISONS CHAWAPA HASIRA