Home Uncategorized SUALA LA VAR AFRIKA NI PASUA KICHWA

SUALA LA VAR AFRIKA NI PASUA KICHWA

TIMU ya Esperance imetwaa ubingwa wa klabu bingwa Afrika kwenye mchezo wa fainali ya pili dhidi ya Wydad Casablanca baada ya Wydad kugoma kuendelea na mchezo huo dakika ya 62 kwa kutokubaliana na maamuzi ya mwamuzi.
Kwenye mchezo huo ambao ulikuwa na ushindani mkubwa, Wydad walisawazisha bao walilofungwa na mwamuzi akalikataa kwa kudai wameotea jambo ambalo wachezaji hawakukubali na kuomba mwamuzi akatazame VAR ili kujiridhisha.
 Waamuzi wa mchezo huo hawakujua kwamba VAR ni mbovu hivyo walipotoa taarifa hiyo wachezaji wa Wydad wakaamini kwamba wanaonewa makusudi kwani mchezo wao wa kwanza mwamuzi aliyewaamua alifungiwa na Caf kwa kuchezesha chini ya kiwango. 
Licha ya jitihada za Rais wa Caf, Ahmad Ahmad kuzungumza na mabosi wa pande zote hazikuzaa matunda. 
Refa wa kati aliwaamuru warudi uwanjani wakagoma kurejea uwanjani na kwenda kwenye vyumba vya kubadilishia nguo hali iliyofanya mabingwa kutangazwa kuwa Esperance.
 Wydad wanaamini kwamba bao lao la kusawazisha dakika ya 59 lililofungwa na Walid el Karti na kuzama wavuni lilikuwa halali hivyo hawana imani na mwamuzi.
Hii inakuwa ni mara ya kwanza kwa mchezo wa fainali kushindwa kumalizika baada ya miaka 55 ya historia ya mashindano ya Afrka kwenye michezo ya nyumbani na ugenini. 

SOMA NA HII  SIMBA KUSHUSHA MTAMBO HUU MABAO KUTOKA CONGO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here