Home Uncategorized TIBOROHA ATANGAZA WASIWASI YANGA

TIBOROHA ATANGAZA WASIWASI YANGA


Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Yanga, Jonas Tiboroha, amesema ana wasiwasi na klabu hiyo kama itafabya vizuri katika Ligi ya Mabingwa Afrika.

Tiboroha ametoa kauli hiyo baada ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kuongeza idadi ya timu shiriki katika michuano hiyo kutoka mbili mpaka nne.

Kutokana na ongezeko hilo, Tiboroha anaamini Yanga haiwezi kupata nafasi hiyo kwani ndiyo kwanza inajipanga kwa kuboresha kikosi kutokana na usajili unaofanyika hivi sasa.

Ikumbukwe Yanga imepata bahati hiyo ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya ongezo la pointi zilizoibeba ikichagizwa na kufanya vema kwa Simba kwenye msimu huu.

“Bado Yanga haiwezi kufanya vema maana ndiyo kwanza kikosi kinaboreshwa.

“Kwetu ni jambo la faraja juu ya kuongezwa kwa timu maana itasaidia zaidi kukutangaza na kukuza soka letu.”

SOMA NA HII  GAMONDI PRESHA TUPU, BAADA YA WABONGO KUMGEUZIA KIBAO YANGA