Home Uncategorized WAKATI IKIELEZWA ANATANGAZWA SIMBA LEO, YANGA WAJA NA MPYA JUU YA AJIBU

WAKATI IKIELEZWA ANATANGAZWA SIMBA LEO, YANGA WAJA NA MPYA JUU YA AJIBU


UONGOZI wa Klabu ya Yanga umethibitisha kuwa bado unamuhitaji kiungo wao mshambuliaji, Ibrahim Ajibu na kilichobakia ni yeye kuamua lini asaini mkataba wa kuendelea kukipiga Jangwani.

Kauli hiyo imekuja ni baada ya tetesi kuzagaa kuwa Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amekataa usajili wa Ajibu na kudai hayupo kwenye mipango yake.

Baada ya tetesi hizo, zikazuka nyingine kuwa tayari amemalizana na Simba na kusaini mkataba wa miaka miwili ya kuichezea timu hiyo kwenye msimu ujao.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Mwakalebela alisema tayari wameshazungumza na Ajibu na kufikia muafaka mzuri wa kuendelea kubaki Yanga na yeye ndiye anayechelewesha kusaini.

Mwakalebela alisema tayari mkataba wake umeshaandaliwa, ni baada ya benchi la ufundi la Yanga linaloongozwa na Zahera lililoshirikisha viongozi
waliokubaliana kwa pamoja kumbakisha Ajibu.

“Hakuna asiyefahamu uwezo, kiwango na mchango mkubwa alioutoa Ajibu kwenye msimu uliopita wa ligi, ni kati ya wachezaji waliofanikisha Yanga kumaliza ligi tukiwa katika nafasi ya pili, licha ya kukubaliana na changamoto mbalimbali.

“Hivyo, kama uongozi tumekubaliana kwa pamoja kuhakikisha tunaikamilisha ripoti ya kocha aliyoitoa kwa viongozi na kikubwa ni kuhakikisha tunambakisha Ajibu Yanga,” alisema Mwakalebela.

SOMA NA HII  KATAKATA YAPITA YANGA,HUYO LUIS ANA BALAA, NDANI YA CHAMPIONI JUMATANO