Home Uncategorized WAKILI WA WAMBURA ACHACHAMAA BALAA

WAKILI WA WAMBURA ACHACHAMAA BALAA


WAKILI wa Michael Wambura, Fatius Kamugisha ameiomba mahakama kuharakisha uchunguzi wa kesi ya mteja kwa kuwa amekuwa ndani kwa muda na kukosa haki zake za msingi.

Katika kesi ya msingi, kigogo huyo anakabiliwa na mashtaka 17, likiwamo la kughushi, shtaka moja la kutoa na kuwasilisha nyaraka za uongo, mashtaka 13 ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na mawili ya kutakatisha fedha haramu.

Wakili Kamugisha aliiambia mahakama kuwa Wambura anakosa haki zake za msingi hivyo ni vyema uchunguzi ukaharakishwa ili kujua hatma ya mteja wake.

Kamugisha ambaye anamuwakilisha wakili wa Wambura Majura Magafu alisema Wambura yupo ndani lakini bado haijathibitika kweli alifanya hayo wanayomshitaki au la hivyo ni vyema uchunguzi ukakamilika na kesi kuanza kusikilizwa.

Wakili wa Serikali, Maghesa Ndimbo aliiambia mahakama kuwa uchunguzi kwa upande wao anaendelea na bado nyaraka zipo kwa mtaalamu wa maandishi anapitia ripoti kwa sasa.

Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu alisisitiza kuwa serikali iharakishe uchunguzi wake. Hakimu huyo aliahirisha kesi hiyo mpaka Juni 18, mwaka huu. Wambura anaendelea kuwa rumande kutokana na kutokuwa na dhamana.

SOMA NA HII  SIMBA WAIVUTIA PUMZI UD SONGO, MAKALI YAO YOTE KWA AZAM FC