Home Uncategorized Wakimataifa ni wanne msimu wa 2019/2020

Wakimataifa ni wanne msimu wa 2019/2020

Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limethibitisha Tanzania kuwa. A timu nne (4) katika maahindano ya Kimataifa kwa msimu wa 2019/2020.
Kwa taarifa hii inamaana timu mbili zitashiriki ligi ya mabingwa na mbili nyingine kombe la shirikisho.

Nafasi hii imekuja baada ya Tanzani kushika nafasi ya 12 katika viwango vya ubora vya CAF.

Kwa mujibu wa kanuni za Ligi zilizofanyiwa marwkebisho na kamati ya utendaji baada ya kupatikana nafasi nne, timu za Tanzania zitakazoshiriki katika mashindano hayo ni Simba Sc na Young Africans Sc (Yanga) katika Ligi ya Mabingwa, Azam Fc na KMC katika kombe la shirikisho.

# Timu P GD Pts
1 Simba SCSimba SC 38 62 93
2 Yanga SC 38 29 86
3 Azam FC 38 33 75
4 KMC FC 38 15 55

KMC atawakilisha kombe la Shirikisho kwa mujibu wa kanuni hiyo ambayo inatamka kama timu iliyomaliza nafasi ya tatu ndio bingwa wa kombe la FA basi mshindi wa 4 anapata nafasi ya kucheza shirikisho, kwa sababu bingwa wa FA anawakilisha nchi kwenye mashindano hayo.

Taarifa pia inasema Caf imeshafungua dirisha la usajili kwaajili ya mashindano hayo, mwisho wa usajili ni juni 30, 2019


Msimu wa 2019/2020 ni msimu wa burudani tele kwa wapenzi wa Kandanda nchini, hizi taarifa umezipokeaje? Tupe maoni yako

The post Wakimataifa ni wanne msimu wa 2019/2020 appeared first on Kandanda.

SOMA NA HII  MHALIFU ALIYEWAPIGA WANAHABARI MIKWARA, AIBUKA NA NYINGINE KALI MAHAKAMANI LEO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here