Home Uncategorized YANGA YAIKOMALIA SAINI YA NYOTA HUYU, IKITIKI BASI WANAKUWA NA VIUNGO WANNE...

YANGA YAIKOMALIA SAINI YA NYOTA HUYU, IKITIKI BASI WANAKUWA NA VIUNGO WANNE MATATA

UNAAMBIWA kama Yanga itakamilisha usajili wa kiungo wa Kagera Sugar, Kassim Khamis basi watakuwa wana viungo wakali wanne ambao wanatoka visiwani Zanzibar.

Khamis ni nyota wa timu ya Taifa ya Zanzibar kwa sasa anakipiga Kagera Sugar akiwa na mabao 7 kwenye ligi aliyofunga.

Kocha wa Kagera Sugar, Mecky Maxime amesema kuwa viongozi wa Yanga wanahitaji saini ya mchezaji huyo kwa kuwa walimfuata.

“Kuna kiongozi wa Yanga alinifuata na kuniambia anahitaji nimpatie mchezaji wangu Khamis, nimemwamba atulie kwanza tukamilishe mipango ya mwisho,” amesema Maxime.

Endapo Yanga watapata saini ya Khasim watakuwa na jumla ya viungo wanne wenye asili ya Zanzibar ambao ni pamoja na Feisal Salum ‘FeiToto’, Mohamed Issa ‘Banka’ pamoja na Abdul Aziz Makame ambaye inaelezwa ameshasasini.

SOMA NA HII  LEBO ZA KIMATAIFA, KIBA ANAKWAMA WAPI?