Home Uncategorized ZAHERA ABADILI GIA YA USAJILI YANGA AKIWA MISRI

ZAHERA ABADILI GIA YA USAJILI YANGA AKIWA MISRI


VIONGOZI wa Klabu ya Yanga chini ya mwenyekiti wake, Dk Mshindo Msolla, wikiendi hii waliitumia kwa ajili ya kuzungumza na wachezaji waliopo ndani ya kikosi hicho ambao mikataba yao inamalizika.

Yanga hadi sasa tayari wameshatambulisha nyota 10 wapya ambao wamewasajili ndani ya kikosi hicho kwa msimu ujao ambao ni pendekezo la kocha wao mkuu, Mwinyi Zahera.

Kwa sasa Yanga wanazungumza na wachezaji hao ambao mikataba yao imemalizika ikiwemo Raphael Daud, Abdallah Shaibu ‘Ninja’ na Mrisho Ngassa ambao Zahera amependekeza wabakie.

Makamu mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela ameliambia Championi Jumatatu, kuwa wamefikia hatua hiyo baada ya kumaliza maagizo ya Zahera juu ya kusajili nyota wa kimataifa na wazawa walio timu nyingine.

“Wiki hii tulikuwa na mazungumzo na wachezaji waliopo ndani ya timu ambao mikataba yao imeisha kwa ajili ya kuendelea kubakia kwenye timu kwa msimu ujao.

“Tumeanza hivyo kutokana na mapendekezo ya kocha Zahera baada ya kuona tumemaliza usajili wa nyota wa kimataifa na wale wa ndani ya nchi ambapo tumebakiza wachache tu. “Wachezaji hao tunaofanya nao mazungumzo ni wale kocha ambao amesema wabaki pekee, zoezi letu sisi tunalikamilisha karibuni na tukimaliza basi tutangaza,” alisema Mwakalebela

SOMA NA HII  ZAHERA AMPA YONDANI KITAMBAA CHA AJIBU