Home Uncategorized ZAHERA ATAJA SABABU NYINGINE YA KUFUNGWA NA OKWI, AWATAJA CAF

ZAHERA ATAJA SABABU NYINGINE YA KUFUNGWA NA OKWI, AWATAJA CAF


BAADA ya timu ya taifa ya DR Congo kupokea kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa Uganda, juzi Jumamosi, Kocha Msaidizi wa DR Congo, Mwinyi Zahera amesema kuwa chanzo cha kipigo hicho ni uchovu walioupata siku moja kabla ya mchezo huo.

Kikosi hiko cha DR Congo ambacho kimejaa mastaa, kimejikuta kikichezea kichapo hicho katika mchezo wao wa kwanza wa Kundi A katika michuano ya Kombe la Mataifa Afrika (Afcon) inayoendelea nchini Misri huku mashabiki wengi wakiwa hawategemei matokeo ya aina hiyo.

Katika mchezo huo moja ya mabao ya Uganda yalifungwa na Emmanuel Okwi ambaye ni mchezaji wa Simba na amekutana na Zahera mara kadhaa katika majukumu ya ngazi ya klabu kwa kuwa Zahera ni kocha wa Yanga.

Zahera amesema: “Siku moja kabla ya mechi hii, tulitumia muda mwingi hospitalini tukifanyiwa vipimo kuanzia asubuhi mpaka saa nne usiku, haikuwa sahihi kabisa, waandaaji wamekosea sana.

“Hicho ndicho kilisababisha kutupa uchovu uliopelekea kupoteza mechi ya kwanza dhidi ya Uganda kwani wachezaji walikosa muda mzuri wa kupumzika.” Kikosi hicho cha DR Congo ambacho kinanolewa na Kocha Mkuu wa AS Vita, Florent Ibenge akisaidiwa na Zahera ambapo kwa sasa kinaburuza mkia katika Kundi A.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMATANO