Home Uncategorized BAADA YA KUMALIZANA NA SIMBA, KAHATA ATOA TAMKO

BAADA YA KUMALIZANA NA SIMBA, KAHATA ATOA TAMKO


Baada ya kumalizana na Simba kwa kusaini mkataba wa miaka miwili, kiungo wa zamani wa Gor Mahia FC, Francis Kahata, amefunguka kuhusiana na Meddie Kagere.

Kahata amesema kuwa utakuwa ni wakati mzuri kwake kuwa timu moja na Kagere ambaye walicheza pamoja enzi wakiwa Gor Mahia FC.

“Ni raha sana kujiunga tena na Kagere ambaye nilikuwa na wakati mzuri sana nae tulipokuwa Gormahia, ni straika mzuri sana na nadhani kucheza nae Simba itakuwa hamasa kubwa sana kwangu,”aliongeza Kahata ambaye hata kiungo wa zamani wa Simba, Hillary Echessa amekiri kwamba Mnyama atatisha.

Kahata tayari alikuwa amemaliza mkataba wake na Gormahia ambayo ni miongoni mwa klabu kongwe za Kenya ambazo inadaiwa zimeyumba kiuchumi na sasa atakuwa Simba kwa misimu miwili ijayo.

SOMA NA HII  MAJEMBE YA KAZI KWA YANGA NA SIMBA YANAYOANDALIWA KWA DABI NOVEMBA 7