Home Uncategorized BALINYA APEWA DAWA YA KUIMALIZA SIMBA HARAKA

BALINYA APEWA DAWA YA KUIMALIZA SIMBA HARAKA


Wakati uongozi wa Yanga ukiwa katika harakati zake za kukisuka upya kikosi chake kwa ajili ya msimu ujao, mshambuliaji mpya wa timu hiyo, Juma Balinya amepewa dawa ya kuitandika Simba kila atakapokuwa akikutana nayo uwanjani.

Balinya aliyesajiliwa na Yanga hivi karibuni akitokea Polisi FC ya nchini Uganda, dawa hiyo amepewa na aliyekuwa mshambuliaji wa Yanga, Mrundi Amissi Tambwe ambaye kwa sasa yupo kwao nchini Burundi ambako amerudi baada ya mkataba wake na Yanga kufikia tamati.

Tambwe alisema kwa jinsi Balinya anavyocheza ana uhakika atakuwa mrithi wake sahihi pia anaamini atayaendeleza mazuri yote ambayo ameyafanya akiwa na klabu hiyo.

“Jambo kubwa ambalo kama nitapata nafasi ya kukutana naye, nitamshauri, kuwa makini katika kutimiza maagizo ya kocha kama ambavyo mimi nilikuwa nikifanya.

“Naamini kabisa akifanya hivyo, atakuwa ni mwiba mchungu kwa timu mbalimbali za ligi kuu ikiwemo Simba ambayo pia nilikuwa nikiitesa.

“Lakini pia, mabeki wa kati wa Simba ambao wapo kwa sasa wengi wao kasi yao pia imepungua na hawana uwezo wa kupambana,” alisema Tambwe.

SOMA NA HII  UNAAMBIWA HUYO YAO HAPO JANGWANI NI ZAIDI YA JESHI