Home Uncategorized CAF YAFANYA MABADILIKO KWA MECHI ZA LIGI YA MABINGWA AFRIKA, SIMBA NA...

CAF YAFANYA MABADILIKO KWA MECHI ZA LIGI YA MABINGWA AFRIKA, SIMBA NA YANGA KAZI KWENU


Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) limefanya mabadiliko ya mechi za mashindano makubwa.

Mabadiliko hayo ni kuanzia msimu ujao wa 2019/20 ambapo limepitisha maamuzi ya mechi za fainali kombe la Shirikisho (CAF Confederation Cup) na klabu bingwa Afrika (CAF Champions League).

Kilichobalika ni kuchezwa mechi moja tu badala ya mechi mbili za nyumbani na ugenini.

Aidha, mechi hizo za fainali zitachezwa katika uwanja huru kwa timu zote zinazofika fainali.

Mabadiliko haya ni sawa na namna mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika pamoja na UEFA Europa League namna yanavyofanyika.

SOMA NA HII  DILUNGA AWAOMBA RADHI MABOSI WAKE WA ZAMANI MTIBWA BAADA YA KUWATUNGUA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here