Home Uncategorized COASTAL UNION YAUPIGIA HESABU KALI MSIMU UJAO

COASTAL UNION YAUPIGIA HESABU KALI MSIMU UJAO



KOCHA Mkuu wa Coastal Union, Juma Mgunda amesema kuwa msimu ujao watapambana kupata matokeo chanya kwenye michezo yao yote.

Akizungumza na Saleh Jembe, Mguda amesema kuwa wanatambua msimu ujao utakuwa mgumu hivyo hesabu kubwa ni kujipanga vema.

“Tunajua kwamba msimu ujao hautakuwa mwepesi nasi tumejipanga kufanya vema, mashabiki waendelee kutupa sapoti kwani tuna kazi ngumu ya kufanya,” amesema Mgunda.

SOMA NA HII  YANGA WAFUNGUKIA HATMA YA JUMA ABDUL NA YONDANI