Home Uncategorized FUKUTO LA MO NDANI YA SIMBA LIMEFIKIA HAPA

FUKUTO LA MO NDANI YA SIMBA LIMEFIKIA HAPA


BAADA ya kuzuka ghafla kwa taarifa kuwa ndani ya uongozi wa Klabu ya Simba hakuna maelewano huku ikidaiwa mwekezaji klabuni hapo, Mohammed Dewji ‘Mo’ kuwa mbioni kung’atuka, Crescentius Magori amefunguka kila kitu.
Taarifa za Mo kutaka kuondoka Simba zilianza kusambaa mitandaoni kuanzia Alhamisi lakini hakukuwa na kiongozi yeyote wa timu hiyo aliyeitisha mkutano wa wanahabari kwa ajili ya kuweka wazi nini kinaendelea.
Kitendo cha Mo Dewji kuandika ‘caption’ za mafumbo kwenye mitandao yake ya kijamii, kilizidi kuwavuruga wanachama na mashabiki wa klabu hiyo ambayo imetwaa ubingwa wa ligi kuu mara mbili mfululizo.
Championi Jumamosi, lilifanikiwa kuzungumza na Magori ambaye ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba kuhusiana na ishu hiyo ambapo alisema, kwa sasa hakuna tatizo lolote ndani ya timu hiyo na kwamba kila kitu kinakwenda sawa kama walivyopanga.
“Hakuna mgogoro wowote ndani ya Simba, kwa sasa kila kitu kinakwenda kama ambavyo kimepangwa, mashabiki wa Simba wanapaswa watulie wasifuate taarifa ambazo hazina ukweli,” alisema Magori.
Naye Mwenyekiti wa Simba, Suedy Mkwabi alisema: “Kwa sasa nipo nchini China, nashughulikia masuala ya biashara zangu, hivyo masuala ya migogoro ndani ya Simba mimi sifahamu, najua kwamba kila kitu kipo sawa.”
Kupitia kwenye ukurasa wake wa Instagram, Mo Dewji, jana aliandika kwamba: “Kwenye uongozi na kwenye maisha, huwa nakaribisha kukosolewa. Lakini siwezi na sikubali kufanya kazi na mtu anayehujumu malengo, mipango na maslahi mapana ya taasisi, mtu anayetoboa mtumbwi tunaosafiri nao.”
SOMA NA HII  KOCHA NAMUNGO ANUKIA MTIBWA SUGAR