Home Uncategorized HICHI NDICHO KILICHOMPA SHAVU BILAL ALLIANCE

HICHI NDICHO KILICHOMPA SHAVU BILAL ALLIANCE


ATHUMAN Bilal ndiye mrithi wa mikoba ya Malale Hamsin aliyekuwa anakinoa kikosi cha Alliance FC.

Mwenyekti wa Kamati ya mashindano ya Alliance, Yusuph Budod amesema kuwa wamekubaliana kamati na kukubali uwezo wa Bilal hali iliyofanya wampe kandarasi ya kukinoa kikosi hicho msimu ujao na atasaidiana na wengine ambao ni Kessy Mziray na Gilbert Dady.

“Tunaamini uwezo wa Bilal hasa ukizingatia alifanya vizuri alipokuwa na timu ya Stand United, imani yetu ni kuona anafanya maajabu msimu ujao,” amesema.

Bilal alikuwa kocha wa Stand United ambayo imeshuka daraja na msimu ujao itashiriki Ligi Daraja la Kwanza.

SOMA NA HII  MGOMBEA SIMBA APEWA MILIONI