Home Uncategorized KOCHA STARS: MAJEMBE YA KAZI YAPO SAWA, AWAPA TANO NYOTA WA SIMBA

KOCHA STARS: MAJEMBE YA KAZI YAPO SAWA, AWAPA TANO NYOTA WA SIMBA

KESHO timu ya Taifa ya Tanzania ‘Tiafa Stars’ itakuwa kazini kumenyana na timu ya Kenya na tayari kambi imenoga na leo ni siku ya maoezi ya mwisho kabla ya mchezo kuchezwa.

Kuungana kwa wachezaji wa Simba ambao walikuwa nchini Afrika Kusini kumeongeza nguvu ndani ya kikosi hicho.

Kaimu kocha mkuu wa Stars, Ettiene Ndayiragije amesema: “Wachezaji hawa wa Simba wako vizuri, nimewaona wakifanya vizuri na tunaendelea kuwajenga ili tushinde mechi hiyo.
“Hii ni nafasi yetu sisi kulipiza kisasi kwao baada ya kupoteza kule Misri ambapo tulipotea kidogo tu, ninaamini kwamba kwa jinsi tulivyo, basi tutafanya vizuri mechi hiyo.”
“Hadi sasa mchezaji Mudathir Yahya hatakuwepo kwa sababu hajafanya mazoezi na wenzake na bado ana maumivu, lakini wengine wote wapo vizuri kwa ajili ya mechi hiyo.”

 Stars itavaana na Kenya Jumapili Uwanja wa Taifa, Dar kabla ya marudiano Agosti 4 nchini humo.

Wachezaji wa Simba waliojiunga na Stars ni pamoja na John Bocco, Ibrahim Ajibu, Jonas Mkude, Aishi Manula, Gadiel Michael, Hassan Dilunga na Erasto Nyoni.
SOMA NA HII  BIASHARA UNITED KUMALIZANA NA JKT TANZANIA LEO