Home Uncategorized KOCHA YANGA ASHINDWA KUJIZUIA, ATOA TAMKO JUU YA WABRAZIL SIMBA

KOCHA YANGA ASHINDWA KUJIZUIA, ATOA TAMKO JUU YA WABRAZIL SIMBA


Kocha wa timu ya wanawake ya Yanga, Mohamed Hussein ‘Mmachinga’, amesema kuwa wachezaji wote wa kigeni ambao wamesajiliwa na Simba, wataibeba timu hiyo kimataifa ila ndani ya Ligi Kuu Bara itakuwa pasua kichwa.

Kwa sasa tayari Simba imemalizana na wachezaji wanne wa kigeni ambao wana uhakika wa kuonyesha makeke yao msimu ujao ikiwa ni pamoja na Wilker Henrique da Silva, Gerson Fraga Viera, Tairone da Silva hawa ni raia wa Brazil wamesaini kandarasi ya miaka miwili na Sharaf Eldin Shiboub Ali Abdalrahman raia wa Sudan ambaye amesaini kandarasi ya mwaka mmoja.

“Wachezaji wa kigeni wanaosajiliwa na Simba watakuwa na msaada mkubwa kwenye michuano ya kimataifa kutokana na ubora wa viwanja ambavyo watacheza pamoja na miundombinu ila kwenye ligi ya ndani watapata taabu.

“Ukweli haujifichi hasa ukizingatia ligi yetu miundombinu bado tatizo hivyo wachezaji wengi watafanya vizuri wakiwa Uwanja wa Taifa ambao una hadhi ya kimataifa wakitoka mkoani itawachukua muda kuzoea mazingira, ila ni somo kwa wazawa nao wanapaswa wapambane wasibweteke,” alisema Mmachinga.

SOMA NA HII  NAMUNGO FC: POLISI TANZANIA WATATUSAMEHE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here