Home Uncategorized LIGI KUU BARA KUANZA KUTIMUA VUMBI AGOSTI, ISHU YA VIPORO YAPATA DAWA

LIGI KUU BARA KUANZA KUTIMUA VUMBI AGOSTI, ISHU YA VIPORO YAPATA DAWA


MTENDAJI Mkuu wa Bodi ya Ligi Tanzania, Boniface Wambura amesema kuwa Ligi Kuu Tanzania Bara inatarajiwa kuanza mwezi Agosti 23 mwaka huu na hakutakuwa na viporo kama msimu uliopita.


Wambura amesema kuwa ratiba ya ligi msimu huu imezingatia kalenda ya michuano ya kimataifa hivyo hakutakuwa na viporo.

“Safari hii hatutakubali kuona timu inaweka kiporo na itambuwe kuwa Bodi ya Ligi haiwabani kwa lolote hivyo ni muda wa kila timu kujipanga ili kufanya vema na kabla ya ligi kuanza mchezo wa ngao ya jamii utakuwa kati ya Simba dhidi ya Azam FC,” amesema.
SOMA NA HII  GARETH BALE AUKUMBUKA MPIRA