Home Uncategorized MUVI YA SIMBA NA OKWI YAJA NA JINGINE JIPYA

MUVI YA SIMBA NA OKWI YAJA NA JINGINE JIPYA


Habari za ndani zinasema kwamba Kaizer Chiefs ina asilimia 85 za kumnasa Emmanuel Okwi, lakini Simba wamecharuka na kujipanga kivingine. Simba imeapa kwamba hata kwa kulipa faini ya kuchelewa lazima wahakikishe Okwi anabaki Msimbazi na wataelewana tu ingawa anawapiga chenga.

Okwi kwa sasa yupo na Uganda kwenye Afcon na inadaiwa kwamba ameshasaini mkataba wa awali na Kaizer ambayo imeshamsainisha kiungo Simba yaonyesha jeuri Misri James Kotei.

Mmoja wa viongozi wa Simba aliliambia Spoti Xtra kwamba bado hawajakata tamaa kwa Okwi na wako tayari kulipa hata fainali ya milioni moja Caf jina lake lichelewe.

“Hata kama tutachelewa tutalipa faini lakini lazima tupambane tumalizane nae na tumbakize Simba,”alisema kiongozi mmoja mwenye ushawishi ndani ya Simba ingawa alikiri kwamba Okwi anatikisa kiberiti na kuna uwezekano mkubwa ana ofa ya maana.

Okwi aliiambia televisheni ya SABC ya Afrika Kusini wiki hii kwamba bado hajasaini popote lakini atafanya maamuzi dakika yoyote baada ya kumalizana na Afcon.

Kwa mujibu wa kanuni za Caf mwisho wa kuwasilisha majina ni Julai 11 lakini baada ya hapo kila wiki klabu itakuwa ikilipa faini ya Sh500,000. Mashindano ya Caf yanaanza mwezi Agosti ambapo tayari Tanzania imeshathibitisha ushiriki wa Simba, Yanga kwenye Ligi ya Mabingwa na Azam na KMC kwenye.

SOMA NA HII  JUMA ABDUL AWACHAMBUA MABEKI WA YANGA