NAHODHA wa timu ya Tanzania, Mbwana Samatta amesema kuwa licha ya kupoteza michezo yote waliyocheza kwenye michuano ya Afcon bado anajivunia uwezo wa wachezaji wenzake.
Stars imetolewa kwenye michuano ya Afcon baada ya kucheza michezo yote mitatu bila kujikusanyia pointi huku ikikubali kufungwa jumla ya mabao nane na kufunga mabao mawili pekee.
“Haikuwa lengo letu kufanya vibaya, tulipambana kwa kadri ya uwezo wetu mwisho wa siku tukashindwa, ila ninajivunia uwezo wa wachezaji wenzangu wamefanya kitu kikubwa nina amini wakati ujao tutafanya vizuri,” amesema Samatta.
Stars ilikuwa kundi C pamoja na Kenya, Senegal na Algeria na mbili zilizofuzu hatua ya 16 bora ni Senegal na Algeria.