Home Uncategorized NYOTA MWINGINE YANGA ACHOMOLEWA MAZIMA

NYOTA MWINGINE YANGA ACHOMOLEWA MAZIMA

PIUS Buswita mshambuliaji wa zamani wa kikosi cha Yanga ambaye amepigwa chini kwa sasa amewekwa kwenye rada za timu ya Kagera Sugar na Polisi Tanzania.


Kagera Sugar chini ya kocha Mecky Maxime kwa sasa inaendelea kujisuka upya ambapo tayari imeanza kazi ya kusajili mashine kali kwa msimu ujao ikiwa ni pamoja na Awesu Awesu, Evarigitius Mujwahuki na imemuongezea mkataba beki Juma Nyosso.

Habari zimeeleza kuwa tayari kwa sasa wameanza mazungumzo na mshambuliaji huyo wa zamani wa Yanga na ameshapewa mkataba anachosubiriwa ni yeye kumwaga wino.

Kocha wa Kagera Sugar, Maxime amesema kuwa bado mipango inaendelea hivyo mambo yakiwa sawa kila kitu kitakuwa hadharani.
SOMA NA HII  GEITA GOLD WAPANIA KUSHIRIKI LIGI KUU BARA