Home Uncategorized NYOTA STARS APELEKWA MUHIMBILI

NYOTA STARS APELEKWA MUHIMBILI


MUDATHIR Yahaya nyota wa kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars’ amepelekwa hospitali ya Muhimbili kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Jana Yahaya alikuwa mazoezini alishindwa kufanya kutokana na jeraha alilolipata nchini Misri kwenye michuano ya Afcon.

Kaimu Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa Stars, Ettiene Ndayiragije amesema kuwa wameamua kumpeleka Muhimbili ili kumfanyia uchunguzi zaidi.

“Mudathir alipata majeraha huko Misri kwenye AFCON, tulimpa muda wa kupumzika, hakuwa sehemu ya kikosi cha Azam kilichoshiriki Kagame na alipojaribu kufanya mazoezi aaihisi maumivu.


“Tunampeleka Muhimbili kwa uchunguzi zaidi kwa sababu ili apate matibabu haraka na kurejea kwenye ubora wake,” amesema. 

Stars ipo kambini kwa ajili ya maandalizi ya michuano ya Chan na mchezo wa kwanza utachezwa uwanja wa Taifa, Julai 28.

SOMA NA HII  ISHU YA WACHEZAJI WANAOPIGWA PANGA NDANI YA SIMBA IMEFIKIA HAPA