Home Uncategorized NYOTA WA SIMBA KUTIMKIA SINGIDA UNITED

NYOTA WA SIMBA KUTIMKIA SINGIDA UNITED

NYOTA wa Simba, Marcel Kaheza ambaye mkataba wake na AFC Leopards ya Kenya alikokuwa kwa mkopo umemalizika kwa sasa ameingia rada za Singida United ambao wanasuka kikosi upya.

Hesabu za Singida United zilikuwa kuipata saini ya mshambuliaji Rashid Juma kutokana na ugumu wa kumpata nyota huyo wameshusha majeshi yao kwa Kaheza.

Ofisa Habari wa Singida United, Cales Katemana amesema kuwa mpango wa usajili kwa sasa ndani ya Singida United umepamba moto hivyo kama jina la nyota huyo limo kwenye ripoti ya mwalimu watamnasa.

“Tunasajili kwa mapendekezo ya mwalimu hivyo kama atatuambia tumsajili Kaheza tutazungumza naye kwani hakuna kinachoshindikana kikubwa ni kuwa na timu bora itakayoleta ushindani,” amesema.

SOMA NA HII  BEKI HUYU CHIPUKIZI AINGIA ANGA ZA SIMBA