Home Uncategorized SABABU YA YANGA KUWEKA KAMBI MAPEMA MORO YATAJWA

SABABU YA YANGA KUWEKA KAMBI MAPEMA MORO YATAJWA


UONGOZI wa Yanga umesema kuwa umeanza maandalizi ya Ligi mapema ili kuandaa kikosi kitakacholeta ushindani msimu ujao.


Akizungumza na Saleh Jembe, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela amesema kuwa kwa sasa wachezaji wameanza kambi mkoani Morogoro kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao.

“Wachezaji wa Yanga kwa sasa wameingia kambi ambayo inafanyika Morogoro na ni maalumu kwa ajili ya kuandaa kikosi bora kitakacholeta ushindani msimu ujao,” amesema.

Yanga msimu uliopita walimaliza Ligi Kuu Bara wakiwa nafasi ya pili ambayo imewapa tiketi ya kushiriki michuano ya kimataifa baada ya Simba kufanya vema michuano hiyo.
SOMA NA HII  KIKOSI CHA SIMBA KITAKACHOANZA LEO DHIDI YA TANZANIA PRISONS, ILANFYA NDANI