Home Uncategorized SIMBA KUKIPIGA NA ARSENAL KWA MKAPA

SIMBA KUKIPIGA NA ARSENAL KWA MKAPA


Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Klabu ya Simba na mwekezaji wa Klabu hiyo, Mohammed Dewji ‘Mo’, ameonekana akiwa na jezi ya Timu ya Arsenal ambayo imesainiwa na wachezaji huku akiishukuru timu hiyo kubwa duniani.

Mo kupitia akaunti yake ya Instagram, ameandika ujumbe wa kuishukuru Arsenal inayoshiriki Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) kwa zawadi hiyo huku akisema kuwa anatarajia kuwa nao hapa nchini hivi karibuni,  jambo ambalo hajaainisha iwapo Arsenal itatua Tanzania hivi karibuni kwa ajili ya ziara ama mchezo.

Mo ameandika;

“Asante @Arsenal kwa jezi iliyosainiwa! Natarajia kutafuta njia za ushirikiano na @SimbaSCTanzania. Tunataraji kuwa nanyi Tanzania hivi karibuni. !,” ameandika Mo.

Kila Agosti 8 ya kila mwaka Klabu ya Simba hufanya bonanza linalojulikana kama #SimbaDay ambapo hucheza na timu kutoka nje ya Tanzania, kuwatambulisha wachezaji wao wapya kwa ajili ya msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara na Mashindano ya Kimataifa.

SOMA NA HII  JAMES KOTEI ATAJWA KUMALIZANA NA YANGA MIAKA MIWILI