Home Uncategorized STRAIKA MPYA KMC AJA NA MKWARA KWA KAGERE

STRAIKA MPYA KMC AJA NA MKWARA KWA KAGERE


Baada ya mshambuliaji mpya wa KMC, Salim Aiyee kutupia bao katika mechi ya kwanza ya michuano ya Kagame, sasa ametamba kufunga pia kwenye mchezo wa kwanza wa ligi kuu.

Aiyee ameifungia timu yake bao kwenye mechi dhidi ya Atlabara FC ya Sudan ambapo mechi hiyo
ilimalizika kwa sare ya bao 1-1, Jumapili iliyopita.

Aiyee ameliambia Championi Jumatano kuwa, anataka kuweka rekodi ya kufunga bao kwenye mechi ya kwanza ya ligi kama alivyofanya kwenye michuano ya Kagame inayoendelea nchini Rwanda.

“Nahitaji kufunga bao kwenye mechi ya kwanza ya ligi kama nilivyofanya huku kwenye michuano ya Kagame, kufunga mabao ni kazi yangu hivyo natakiwa nifunge bila kuchoka,” alisema Aiyee.

Aiyee aliongeza kuwa amepania kuivunja rekodi ya mabao 23 yaliyofungwa na mshambuliaji wa Simba, Meddie Kagere.

“Kagere alifunga mabao 23, nahitaji kufunga zaidi ya pale maana naamini nikifunga mabao zaidi ya 23 nitaisaidia sana timu yangu ya KMC pamoja na mimi mwenyewe,” alisema Aiyee.

KMC inatarajiwa kucheza mechi yake ya kwanza ya Ligi Kuu Bara msimu ujao dhidi ya Azam FC Agosti 29, mwaka huu.

SOMA NA HII  HAWA NDIO ANGUKO LA GAMONDI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here