Home Uncategorized TANZANIA YAWALILIA WAANDISHI WATANO WALIOTANGULIA MBELE ZA HAKI KWA AJALI

TANZANIA YAWALILIA WAANDISHI WATANO WALIOTANGULIA MBELE ZA HAKI KWA AJALI

OFISA Mtendaji Mkuu wa Azam Media, Tido Mhando amesema kuwa ni ngumu kuamini juu ya safari ya wafanyakazi wenzake ambao wamefariki kwa ajali ila kazi ya Mungu haina makosa.

Jana wafanyakazi watano wa Azam Media Group walifariki baaada ya kupata ajali ya gari iliyotokea maeneo ya kati ya  Shelui (Mkoani Singida) na Igunga, Tabora.

Waliotangulia mbele za haki ni pamoja na Charles Wandwi, Florence Bitaliho, Said Hassan, Salum Mhando na Silvanus Mhando.

Leo wameagwa na kupumzishwa kwenye makazi yao ya milele na maelfu ya watu ambao wamejitokeza kwenye msiba huu ambao umegusa hisia za watanzania wengi.

SOMA NA HII  HESABU ZA SIMBA KWA SASA NI LIGI YA MABINGWA AFRIKA